'Aunt Ezekiel hataki tena mambo ya kitoto'

09Jan 2017
Sabato Kasika
Dar es Salaam
Nipashe
'Aunt Ezekiel hataki tena mambo ya kitoto'

NYOTA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ameamua kubadili mtindo wake wa maisha kwa kuachana na mambo aliyoyaita ya kitoto, kwa madai kwamba kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.

Aunt Ezekiel.

Alisema Aunt Ezekiel wa sasa siyo yule wa miaka ya nyuma aliyekuwa akijichanganya katika mambo mbalimbali na kwamba sasa amekuwa mtu mzima anayefanya kila kitu kwa umakini.

"Nimeamua kubadili mtindo wangu wa maisha kwa kuachana na mambo yote ya kitoto kwani ninaamini kwamba kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho," alisema msanii huyo alipozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki.

Msanii huyo ambaye amekuja na filamu mpya iitwayo 'Christmas Eve' aliyoigiza akitumia jina la Salome, aliwataka mashabiki wa Bongo Movies kufuatilia filamu hiyo badala ya kutaka kujua habari zinazohusu maisha yao binafsi na mpenzi wake Iyobo.

Alisema mabadiliko yake hayapo tu kwenye maisha bali hata uigizaji akifafanua kuwa katika filamu hiyo amefanya vitu adimu kwa filamu za Kitanzania.

Habari Kubwa