Ben Pol apata ulaji Ufaransa

10Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Ben Pol apata ulaji Ufaransa

MSANII wa muziki wa bongo fleva , Benard Paul 'Ben Pol' ameenda nchini Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya MAUA itakayofanyika Novemba 18 mwaka huu jijini Paris imeelezwa.

Benard Paul 'Ben Pol'.

Katika ziara hiyo, Ben Pol ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali, pia anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa filamu mpya ijulikanayo kwa jina la Ndoto.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ben Pol, alisema anashukuru kwa kupata mwaliko wa kwenda kuhudhuria uzinduzi huo, lakini pia nafasi aliyopata ya kuwa balodi wa taasisi hiyo ya MAUA.

"Hapa tunapozungumza tayari nimeshafika Paris, nina imani nitafanya mengi ambayo yatasaidia kutangaza kipaji changu katika tamasha hili ambalo ni mara ya kwanza kwangu kushiriki," alisema msanii huyo.

Naye mratibu wa Taasisi ya MAUA, David Shenyagwa, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika na wanatarajia shoo hiyo itahudhuriwa na Wana-Diaspora, viongozi na wageni mbalimbali wanaoishi ndani na jirani mwa jiji hilo la Paris.

Habari Kubwa