Dar kula Krismas wakivunja mbavu

12Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Dar kula Krismas wakivunja mbavu

MSANII wa vichekesho nchini MC Pilipili ameandaa ‘show’ ya kufungia mwaka huku akiwashirikisha wasanii wenzake watano wa vichekesho.

Akizungumza na waandishi wa habari, MC Pilipili alisema kuwa onyesho hilo litafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019.

Alisema wasanii ambao atashirikiana nao kwenye onyesho hilo ni Dogo pepe, Oscar Nyerere, MC Munga, Petit na Katariba wa Karatu.

“Naamini kwa kila mtu atakayekuja kwenye onyesho hilo ataondoka na kitu, nilikaa kimya sana mwaka huu kwa sababu nilitaka kupumzika na kujipanga upya, lakini sasa nipo tayari kuonyesha umahiri wangu kwenye kuchekesha,” alisema MC Pilipili.

Aidha, alisema maandalizi kuelekea kwenye onyesho hilo yanaendelea na litafanyika Kebbys kwenye sikukuu ya Krismas.