Dawa za kulevya zamkera Batuli

26Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
Dawa za kulevya zamkera Batuli

MOJA ya matatizo yanayowakabili vijana nchini ni utumiaji wa dawa za kulevya ambazo zinachangia kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Yobnesh Yusuf 'Batuli'.

Tatizo hili linawakera watu mbalimbali na mmojawapo ni msanii wa Bongo Movie, Yobnesh Yusuf 'Batuli', anaitaka jamii kuunguna na Serikali kupiga vita ya matumizi ya dawa hizo.

"Nilishasema awali, ninaumia sana kuona vijana wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na kuharibu maisha yao na nguvu kazi ya taifa," alisema Batuli.

Msanii huyo alisema kuwa yeye ni mama na kijana anayeumia kuona vijana wenzake wakiwa waathirika wakubwa wa tatizo hili.

"Nakumbuka mwaka jana niliandika ujumbe kwenye mtandao wa jamii nikieleza kukerwa na utumiaji wa dawa hizi. Naumia sana kuona kundi la vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa likijihusisha na utumiaji wa dawa hizo...mimi ni mzazi, tuungane kupiga vita hii," Batuli alisema.

Aliongeza kuwa tatizo la dawa za kulevya ni janga kwa kizazi cha sasa na kwamba waathirika wakubwa ni vijana wanaofuata mkumbo.

Habari Kubwa