Diarra, Lulu, Siti Band wapagawisha sauti za Busara

14Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
ZANZIBAR
Nipashe
Diarra, Lulu, Siti Band wapagawisha sauti za Busara

WASANII nyota kutoka Afrika usiku wa Februari 13 wameweza kukonga nyo kwa mashabiki wa muziki wa mataifa mbalimbali waliojitokeza siku ya kwanza ya tamasha la muziki la Kimataifa la Sauti za Busara.

Wasanii wa kundi la Lulu Abdalla.

Wasanii kutoka visiwani hapa, Siti & the Band waliweza kuonyesha uwezo wao wa kupiga muziki wa asili wa Afrika pamoja na muziki wa mwambao (taarab) na aina ya rege ambao uliamsha shangwe nara zote wa mashabiki wa muziki waliofurika Ngome Kongwe.

 Pia  kundi la Tara Jazz  ambao nao wanatokea visiwani hapa  waliweza kuamsha shangwe kwa nyimbo zao zilizokuwa na mchanganyiko wa afro jazz ya asilia ya kiafrika.

Msanii wa kutoka Kenya, Lulu Abdalla naye aliwasha moto mkali kattika jukwaa hilo alipopanda na bendi yake kwa mziki wa asili ya Afrika uliojaa vionjo mbalimbali vya asili.

Siti & the band.

Msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali kupitia albam yake ya 'Thembassa'  ya 2014,   alipagawisha umati mkubwa.

Mwanadada kutoka Senegal, Thais Diarra aliweza kuonyesha umahiri wake wa kuimba muziki wa uliochanganywa na vionjo vya ala za asili ya Afrika Magharibi. Ndani ya Ngome Kongwe umati mkubwa ulifurika kushuhudia tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la 17 kutokea kuanzishwa kwakwe.

Wasanii wa Tarra Jazz.
Wasanii wa Tarra Jazz.

Habari Kubwa