Dully hana mpango na lebo ya mtu

09Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Dully hana mpango na lebo ya mtu

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, amesema hana mpango wa kujiunga na lebo yoyote ya muziki na badala yake anajiandaa kuanzisha yake itakayosimamia wasanii wachanga.

"Hiyo ni moja ya mipango yangu kwa mwaka 2017 kwani nitaanzisha lebo ikiwa na masharti kidogo kwamba nitakuwa na wasanii wachanga tu wale ambao wananizidi hawatakuwa na nafasi," alisema Dully.

Aliliambia gazeti hili juzi kuwa mipango ya kuanzisha lebo yake ni ya muda mrefu na sasa imekamilika na ndiyo maana tangu aanze muziki hajawahi kujiunga na lebo yoyote licha ya kuombwa kufanya hivyo.

Alisema alianza kwa kuanzisha studio ya kurekodi muziki na kisha akawa na wasanii anaowasimamia, ambao sasa watakuwa chini ya lebo anayotarajia kuanzisha mwezi ujao.

Dully alisema amejipanga kuhakikisha kwamba kile alichokipanga kwa ajili ya maendeleo ya muziki wake katika mwaka 2017 kinatimia, kwa madai kuwa alianza kujipanga muda mrefu.

Habari Kubwa