Kumbe Billnass anapenda wali maharage

15Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kumbe Billnass anapenda wali maharage

MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva ,Faustina Mfinanga maarufu ‘Nandy’ amefunguka chakula anachokipendelea zaidi mpenzi wake Billnas kuwa ni wali maharage nazi.

Mwanamuziki huyo ambaye amelamba dili nono la kuwa balozi wa nazi ya Azania ‘Azania Coconut Cream’amesema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya kutoka katika kampuni ya Azania Group.

“Billnass anapenda sana wali maharage nazi, lakini sitaki sana kutoa siri za ndani asije mtu akapika wali maharage nazi bure ha ha ha ” alisema Nandy.

Nandy alisifia kiungo hicho cha nazi kuwa ni  bora kuliko zingine alizowahi kuzitumia katika mapishi kwa kuwa kina virutubisho vya kutosha.

Habari Kubwa