Linah azikikataa lebo za kitanzania

03Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Lete Raha
Linah azikikataa lebo za kitanzania

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga amesema kuwa kuna lebo nyingi sana zinazotaka kufanya kazi naye, lakini hayuko tayari kwa sababu anajua ugumu wake.

linah sanga.

Alisema kuwa alishapita katika lebo zaidi ya tatu na kushuhudia changamoto zake, hivyo hataki tena kufanya makosa kwa sababu hapendi kuhamahama ndiyo maana anahitaji lebo ambayo atakubaliana nayo kwa kila kitu.

"Sitafanya makosa tena ya kusaini mkataba na lebo yoyote kama nilivyofanya makosa katika kipindi cha nyuma kwani nimeshaona madhara yake, ndiyo maana nikatoa msimamo huo," amesema Linah.

Alisema kuwa kwa mara ya mwisho alikuwa chini ya lebo ya muziki ya ‘Pan Musiq’ na kufanikiwa kufanya miradi kadhaa ikiwamo ya wimbo wa ‘No Stress’, ambao ulichangia kumweka juu.

Kwa sasa mwimbaji huyo ameachia video ya wimbo wake wa ‘Imani’, ambao ni mwendelezo wa kazi zake mpya anazotoa ili kukamilisha albamu ya kwanza kwa mwaka huu wa 2016.

Habari Kubwa