Mc Pilipili kuwania tuzo Nigeria

01Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mc Pilipili kuwania tuzo Nigeria

MSANII maarufu wa vichekesho nchini, Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ amechaguliwa kuwania tuzo ya mchekeshaji bora wa mwaka ya ‘Screama’ zitakazotolewa nchini Nigeria.

Mchekeshaji huyo amekuwa msanii pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo hizo.Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mc Pilipili , alisema kuwa kuteuliwa kwake kuwania tuzo hizo ni ishara kuwa kazi yake inaonekana na kukubalika.

“Kwangu bila kuangalia kama nitashinda tuzo, kuchaguliwa tu kuwania ni ishara kuwa ninafanya kazi nzuri na zinaonekana na kukubalika,” alisema Mc Pilipili.

Alisema kuwa anawaomba Watanzania na wananchi wa Afrika Mashariki kumpigia kura kwa wingi kuweza kushinda tuzo hiyo na kuitangaza Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

 "Nawaomba wana Afrika Mashariki kwa pamoja kunipigia kura katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kufollow

page ya screamawards au screamawards official unatafuta post iliyotumwa   ambayo nipo alafu  unakoment kwa  jina langu MC PILIPILI hapo unakua tayari umenipigia kura," alisema Msanii huyo.

 Alisema katika nchi za Afrika Mashariki kuna wasanii wengi wa vichekesho lakini amekuwa na bahati ya kuwa msanii pekee kuwania tuzo hizo.

Alisema tuzo hiyo wanawania na wasanii wengine11 kutoka katika nchi za Nigeria na Ghana ambapo mshindi wake atatangazwa na kukabidhiwa tuzo kwenye hafla itakayofanyikamapema mwakani. 

Habari Kubwa