Msanii wa Uganda Mozey Radio afariki dunia

01Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Msanii wa Uganda Mozey Radio afariki dunia

Mwanamuziki wa Nchini Uganda, Moses Sekibooga maarufu kwa jina la kisanii Mozey Radio afariki dunia.

Mozey Radio

Meneja wa mwanamuziki huyo, Ballam Barugahara amevieleza vyombo vya habari nchini Uganda kuwa Radio amefariki dunia leo saa 12 asubuhi.Mwanamuziki huyo alikimbizwa Hospitali ya Nsambya siku ya tarehe 23 Januari, 2018 baada ya kuanguka na kuvunjika shingo na fuvu la kichwa wakati akiwa kwenye ugomvi na mlinzi wa ukumbi mmoja wa starehe.

 

Mozey Radio akiwa katika hospitali ya Nsambya.

Hata hivyo Hospitali hiyo haikuweza kumpatia matibabu kutoka na kitengo cha wagonjwa mahututi kujaa ndipo msanii huyo alipo hamishiwa Case Clinic iliyopo Bungando Road Jijini Kampala.

Mwanamuziki huyo ameaga dunia saa kadhaa baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutoa Sh30 milioni kwa ajili ya matibabu yake.

Habari Kubwa