Mzee Yusuph kuja kibongofleva

26Feb 2016
Sabato Kasika
Dar
Nipashe
Mzee Yusuph kuja kibongofleva

MFALME wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amesema amepunguza urefu wa nyimbo zake ili ziendane na wakati.

Mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph.

Mzee alisema kuwa amejifunza mengi baada ya kuwashirikisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika nyimbo zake binafsi na kuona kuna umuhimu wa kubadilika kwa ajili ya kulinufaisha kundi lake.

"Ni muhimu kusoma ishara za nyakati na kufanya kazi kulingana na hali halisi, ndio maana mimi nikaamua kupunguza urefu wa nyimbo zetu mpya zitumie muda sawa na zile za bongofleva," alisema.

Muimbaji huyo alisema kwa muda mrefu tungo zake zilikuwa zinachukua zaidi ya dakika nane lakini ameona ni vyema kubadilika kwa sababu utaratibu huo umepitwa na wakati.

"Nyimbo ndefu zimepitwa na wakati na zinachosha mashabiki," alisema Mzee.

Habari Kubwa