Ray atamani kuwa balozi wa maji

26Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
Ray atamani kuwa balozi wa maji

BAADA ya kueleza kwamba rangi yake nyeupe haitokani na matumizi ya 'mkorogo' na husababishwa na kunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi, msanii nyota wa Bongo Movies, Vincent Kigosi 'Ray' amesema kuwa anatamani kuwa balozi wa maji nchini.

Ray alisema kuwa tangu atoe ufafanuzi huo baada ya 'kushambuliwa' katika wimbo wa 'Shika Adabu Yako' ulioimbwa na Nay wa Mitego kwamba anatumia fedha nyingi kununua vipodozi, anafikiria kufanya mazungumzo na makampuni yanayouza maji ili aweze kuwatangazia biashara hiyo.

"Ninaweza kwenda kampuni yoyote kuomba udhamini nikapata ama kutengeneza makala ya umuhimu wa maji nikapeleka kwenye vituo vya televisheni nikapata fedha, hii itakuwa ni utambulisho wangu pia,"

Habari Kubwa