Rostam lainogesha IOKOTE Tigo Fiesta

21Oct 2018
Na Mwandishi Wetu
Moshi
Nipashe Jumapili
Rostam lainogesha IOKOTE Tigo Fiesta

KUNDI la Rostam linalowashirikisha wasanii wawili Roma na Stamina, jana walipanda jukwaani kuimba pamoja na msanii Maua Sama wimbo unaotamba kwa sasa ujulikanao kama IOKOTE kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika Uwanja wa Majengo mjini Moshi.

wasanii wanaounda kundi la rostam roma pamoja na stamina picha na mtandao

Tukio hilo liliwafanya mashabiki walipuke kwa shangwe kwa namna wasanii wote watatu walivyokuwa wakiiimba kwa pamoja na kufanya kionjo cha aina yake na kwa ubunifu mkubwa.

Hii ilitokea kabla Maua hajashuka jukwaani ndipo Rostam walipovamia jukwaa na kuimba wote, Na mara baada ya kuimba wimbo huo, wakamalizia kuimba wimbo mwingine walioshirikiana uitwao Kibamia.

Tamasha hili likiwa limemaliza mkoa wa sita usiku wa kuamkia jana, baada ya kupita mikoa ya Morogoro, Rukwa, Iringa, Songea, Mtwara na Kilimanjaro.

Wasanii mbalimbali walinogesha tamasha hilo wakiwamo Weusi, Chege, Nandi, Me. Blue,Chin Beez, WhoZu, Rosa Ree, Mavoko na wengine wengi.

Kwa upande wa shindano la kutafuta wasanii wenye vipaji Tigo Fiesta Supa Nyota, msanii anayechipukia, Samson Msweta maarufu kama Samson Classic aliibuka kidedea na atauwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye fainali za Tigo Fiesta Supa Nyota mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Nao wadhamini wa tamasha hilo. Kampuni ya Tigo, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema "mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia.

"Promosheni ya Data Kama Lote, itahakikisha mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+," Bagaka alisema.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi Sh. millioni 10, zawadi za kila wiki za Sh. milioni moja, ama zawadi za kila siku za Sh. 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo.

Habari Kubwa