Ruby: Nina kipaji cha soka, nilicheza Young Twiga Stars

24Jul 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Lete Raha
Ruby: Nina kipaji cha soka, nilicheza Young Twiga Stars

MSANII anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya, Hellen George 'Ruby' amesema kuwa pamoja na kwamba anaimba, ana kipaji kingine alichojaliwa na Mungu cha kucheza soka.

Ruby

Alisema kuwa kabla ya kujulikana kwenye muziki aliwahi kucheza soka katika timu ya Young Twiga Stars lakini baadaye akajikuta amezama moja kwa moja katika upande huu alipo sasa.

"Ninapenda mchezo huu wa soka kwani nilikuwa kuwa katika timu ya Young Twiga Stars, hiki ni miongoni mwa vipaji vyangu ambavyo Mungu amenijalia ingawa sasa ninajulikana zaidi kwenye muziki," alisema Ruby.

Alisema kuwa anatamani japo siku moja ashiriki kwenye mechi moja aonyeshe kipaji chake hicho, kwa vile ana uhakika watu wengi hawajui kwamba alikuwa akicheza soko.

"Kwa hiyo niseme tu kwamba mbali na kuimba muziki wa kizazi kipya, kitu kingine ninachokipenda mchezo wa mpira wa miguu, kwani nina nina kipaji nao ingawa sikuendelea nao," alisema.

Habari Kubwa