Shilole ahukumiwa kulipa faini ya mamilioni

01Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Shilole ahukumiwa kulipa faini ya mamilioni

Msanii wa filamu na muziki nchini, Zuwena Mohamed  maarufu kama ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini na Mahakama ya mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Shilole.

Shilole atakiwa kumlipa faini ya Tsh. Milioni 14  baada ya kupatikana na hatia ya utapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika katika shoo ya muziki iliyoandaliwa na Mary Mussa mnamo mwaka 2017.

Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Machi 1, 2018, imebainika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Tsh. Milioni tatu na  Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mnamo  2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesema Shilole amekuwa akitumiwa wito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi yake lakini amekuwa akikaidi kufanya hivyo hadi mahakama ilipomuandikia wito mwingine kwenye Gazeti la Uhuru lakini hakufika.

Baada ya hukumu hiyo Mahakama imemuamuru Shilole azilipe pesa hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.

 

Habari Kubwa