Shilole kutoka na Man Fongo leo

03Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Lete Raha
Shilole kutoka na Man Fongo leo

KUTOKA ndani ya tasnia ya muziki wa kizazi kipya, msanii Zuwena Mohamed a.k.a Shilole ukipenda muite Shishi Baby amefunguka na safu hii ya Bongo Fleva kwamba leo Jumatano anadondosha ngoma mpya sokoni ikiwa na jina la Mtoto Mdogo akimshirikisha mkali wa Singeli, Man Fongo.

shilole.

Shilole alisema na safu hii juzi kwamba, hana sababu ya kuifagilia kazi hiyo bali anawachia mashabiki wake 'waijaji' ikitoka kwa kuwa shuguli inayofanywa na Man Fongo kwa sasa wengi wanaifahamu huku uwezo wake kwenye muziki ukijulikana.

"Hivi sasa niko vizuri kila idara, kuanzia studio mpaka stejini, nina furaha kubwa kuwaomba mashabiki wangu waipokee ngoma hiyo kwa mikono miwili, najua hawatoniangusha kama mimi nisivyowaangusha kwenye kila wimbo ninaotoa," alisema Shishi.

Mpaka sasa Shilole ameshafanikiwa kuachia ngoma tisa, lakini kwa kuwa soko la albamu haliko poa ameamua kuishi kwa singo moja moja akidai inalipa kuliko albamu ambazo hivi sasa zinaonekana hazina dili kwa sababu wanyonyaji a.k.a mabingwa wa kukopi cd wamekuwa wengi.

Habari Kubwa