Snura: Vyombo vya habari vinaninyima usingizi

24Jul 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Snura: Vyombo vya habari vinaninyima usingizi

STAA wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Snura Mushi ametaja moja ya mambo ambayo yamekuwa yakimnyima usingizi kwamba ni kuandikwa vibaya na baadhi ya vyombo vya habari.

Snura Mushi

Alisema kuwa tangu apate umaarufu ameandika habari nyingi za uongo na kusababisha aumie sana moyoni na kujiuliza amewakosea nini ambao wamekuwa wakimfuatafuata.

"Sipendi kuandikwa habari za uongo kwani huwa ninaumia sana pale ninapoona habari kwenye magazeti zinazonihusu, ambazo mara nyingi huwa hazina ukweli wowote," alisema Snura.

Snura alitolea mfano wimbo wake wa 'Chura' kwamba serikali iliusitisha kwa muda hadi hapo atakapoufanya video nyingine yenye maadili, lakini baadhi ya vyombo vya habari vikaandika kuwa amefungiwa na kwamba huo ulikuwa ni upotoshaji mkubwa.

Habari Kubwa