Wasanii wapata mkombozi wa kazi zao, kusambaza kidigitali

26Jun 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Wasanii wapata mkombozi wa kazi zao, kusambaza kidigitali
  • Boomplay Tanzania kuwawezesha kutatua changamoto zao katika uzalishaji

Wasanii wa Tanzania wamefanya mkutano na Mtandao wa maarufu Afrika wa huduma ya kusikikiza na kupakua muziki( Boomplay Tanzania) lengo likiwa ni kuboresha kazi zao na kuingia katika soko la kimataifa.

Meneja wa boomplay tanzania, Natasha stambuli.

Mkutano huo ulikuwa mahususi kuzungumzia kuhusu kuwezesha wasanii na uzalishaji wa muziki (Production) na usambazaji wa muziki kidigitali (Digital Distribution).

Akizungumza katika mkutano huo Meneja wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli amesema Boomplay inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii kama kupata muda wa studio, "ku-shoot video" zenye ubora wa kimataifa kwa kuliona hilo wameingia mkataba na Wanene Entertainment ili kuwawezesha wasanii kutatua changamoto hizo.

“Barani Afrika Boomplay ina ofisi Tanzania pamoja na Kenya, Nigeria na Ghana. Moja kati ya fursa zinazopatikana ni sisi kuwa na uwezo wa kujenga madaraja kwa wasanii wetu wa Tanzania na wasanii wengine kutoka nchi hizo," Amesema Natasha Stambuli

Amesema katika mkutano huo umejumuisha jopo la wataalamu mbalimbali katika tasnia ya muziki akiwemo Martha Huro, ambaye ni Meneja wa Boomplay Kenya, Lupakisyo Mwambinga, Mkuu wa Idara ya Sheria COSOTA, Nahreel msanii wa bongo fleva kutoka Navy Kenzo, Moses Range, Muanzilishi wa DEMO Innovators, Japhet Kapinga, Meneja Maudhui Boomplay pamoja na msanii wa Hip Hop, Wakazi.

Aidha wasanii na watayarishaji walioshiriki katika mkutano huo walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa wataalamu hao na kupata ujuzi zaidi katika masuala ya sheria, hati miliki, nembo (branding) na vingine vingi katika tasnia ya muziki. 

Habari Kubwa