Wasanii tujitume-Shilole

06Feb 2016
Nipashe
Wasanii tujitume-Shilole

MUIMBAJI wa Bongo Fleva, Shilole, ameonyesha kukua kwa kusema maneno ya busara baada ya kuwashauri wasanii wenzake kuongeza bidii ili kupata mafanikio.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo kinachorishw na EATV, Shilole, alisema hakuna mafanikio yanayokuja bila jasho, lazima kila mtu kuwajibika kama anataka kuwa juu kimuziki.
Alisema yeye anafanya muziki kama ajira yake, hivyo anaheshimu na kutumia akili nyingi kutafakari nini afanye.
“Muziki ni kama kazi yangu, bila kuimba, kucheza, na kutoa video nzuri watoto wangu watakufa njaa, unajua wakati mwingine wasanii wa kike tunajibweteka,” alisema Shilole.

Habari Kubwa