Yamoto wawania kundi bora Afrika

03Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Yamoto wawania kundi bora Afrika

KUTOKA pande za Temeke Mikoroshini, vijana wanne wanaounda kundi la Yamoto Band wameingia kwenye tuzo kubwa za Afrimma zitakazotolewa Marekani Oktoba 15, 2016 wakipambana na makundi mengine kutoka Afrika.

kundi la Yamoto Band.

Akipiga stori na Bongo Fleva, meneja wa kundi hilo, Chambuso alisema kuwa Yamoto wametajwa kuwania tuzo hizo kama kundi bora la muziki kutoka Afrika wakipambana na makundi mengine kutoka Kenya, Uganda, Angola, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana na Congo.

"Tunashukuru Mungu kwa hatua tuliyofikia mpaka hapa tulipo, kundi letu kutajwa kuwania tuzo hizo siyo kitu kidogo, ni heshima kubwa tuliyopewa pia, tunawaomba mashabiki wetu watuombee na kutupigia kura kwa wingi ili tuweze kuiletea nchi yetu sifa kwa kuibuka na ushindi wa tuzo.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliyotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platnumz na Ali Kiba (Msanii Bora wa kiume Afrika), huku Vanessa Mdee na Linah wakiwania tuzo ya Msanii Bora wa Kike kutoka Afrika.

Habari Kubwa