Chanjo polio, surua bado kizungumkuti

13Jan 2016
Nipashe
Chanjo polio, surua bado kizungumkuti
  • "Sisi tunajua umuhimu wa chanjo hizi kwa watoto wetu, tunawaleta hospitali ili wapatiwe lakini serikali sio watiifu, hawasemi ukweli, mara kwa mara wamekuwa wakitusisitizia kuhusu chanjo hizo lakini imeshindwa kutimiza wajibu wao."

LICHA ya serikali kuahidi kuwa chanjo za polio na kifua kikuu zitaanza kupatikana kwenye hospitali zake kuanzia juzi, lakini huduma hiyo bado imeendelea kuwa kitendawili kilichokosa majibu.

waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Nipashe jana ilipita kwenye hospitali za serikali na binafsi na kukuta tatizo la uhaba wa chanjo hizo likiendelea, huku wauguzi wakiwasisitiza wakinamama wenye watoto wanaohitaji huduma hiyo wasubiri hadi tangazo la serikali litakapotoka.
Mmoja wa wa kina mama aliyekutwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Kuruthumu Athumani, alisema ana wiki ya pili sasa mtoto wake mwenye umri wa miezi mitatu hajapatiwa chanjo ya matone ya polio.
Alionyesha kushangazwa na serikali kushindwa kusambaza chanjo kwenye hospitali zake na kusababisha usumbufu mkubwa.
"Sisi tunajua umuhimu wa chanjo hizi kwa watoto wetu, tunawaleta hospitali ili wapatiwe lakini serikali sio watiifu, hawasemi ukweli, mara kwa mara wamekuwa wakitusisitizia kuhusu chanjo hizo lakini imeshindwa kutimiza wajibu wao," alisema Amina.
Kwa Mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Nsachris Mwamwaja, upungufu wa chanjo si kwa nchi nzima ni baadhi ya maeneo na wamekubaliana wale wenye akiba kubwa kuwapelekea walioishiwa.
"Ijumaa iliyopita chanjo za polio ziliwasili za kutosha na sitasambazwa hospitali zote," alisema.

Habari Kubwa