Akihojiwa na chombo kimojawapo cha habari nchini Pinda amesema kuwa ili mgombea ajisifie kushinda ni lazima awepo mtu wa kushindana naye.
"Unajua uzuri wa Chama cha Mapinduzi kina nguvu kubwa sana ,kwa hiyo kama kuna mtu anataka kugombea kwanza anakaribishwa kwa kuwa ni haki yake ,Membe mimi ni rafiki yangu sana" amesema Pinda.
Uchaguzi Mkuu wa Urais wabunge na madiwani unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na tayari vyama mbalimbali vipo katika michakato ya ndani ya kuandaa wagombea wao kwa nafasi mbalimbali.