Akizungumza katika mjadala wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake uliofanyika kwa njia ya mtandao Waziri wa Maji ,Juma Aweso amesema athari hizo zinaweza kukabiliwa kwa uchimbaji wa visima kwa kuwa bado yapo maji chini ya ardhi takriban lita za ujazo bilioni 121.
Sambamba na uchimabaji wa visima Serikali pia imesema itachimba mabwawa na kuboresha mito iliyopo na kusimamia sheria za uthibiti wa mazingira ikiwemo watu kutokufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji.
"Uwezo wa mitambo ya kuzalisha maji Ruvu Juu na Ruvu Chini ni lita Milioni 520, mathalani mtambo wa Ruvu Chini una uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 lakini leo tunapozungumza umezalisha lita milioni 154 kwa hiyo kuna upungufu uliotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi " amesema Aweso.