Bodi ya mikopo yatakiwa kuondoa adhabu ya asilimia 10

04May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Bodi ya mikopo yatakiwa kuondoa adhabu ya asilimia 10

Serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia imeiagiza bodi ya wakurugenzi wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuondoa tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo.

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Mei 4, 2021 na Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Hatua ni kufuatia maagizo ambayo yalitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani alipotaka bodi ya mikopo kushusha kiwango cha tozo na kufikia asilimia sita.

Prof. Ndalichako amesema Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo, itaondolewa kuanzia Julai Mosi 2021.

Habari Kubwa