CAG - Hakuna mkurugenzi ndani ya bodi ya ATCL mwenye ujuzi wa anga

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
CAG - Hakuna mkurugenzi ndani ya bodi ya ATCL mwenye ujuzi wa anga

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL), haina mjumbe mwenye uzoefu wa masuala ya anga, hivyo kusababaishia hasara serikali.

Akiwasilisha ripoti hiyo jijini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 CAG, Charles Kichere amesema “Bodi ya wakurugenzi ya ATCL haina mjumbe mwenye uzoefu na masuala ya anga hivyo inakuwa changamoto kwa ndege kuruka kwenye baadhi ya maeneo, na kukiwa na hasara ya bilioni 150,”

Kichere ameongeza kuwa Bil. 3.92 zilitengwa kama gharama ya matengenezo ya ndege, lakini kazi hiyo haikufanyika.

“Nilibaini kuwa wakala wa ndege za Serikali (TGFA) ililipa Bilioni 3.92 ikiwa ni gharama ya huduma za matengenezo makubwa ya ndege hata hivyo baada ya ziara yangu nilibaini ndege haikuwa ikifanya kazi na ilikuwa imetelekezwa tangu 2015,” amesema.

Habari Kubwa