DC, mkurugenzi Morogoro watumbuliwa

15Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
DC, mkurugenzi Morogoro watumbuliwa

Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwaondoa kazini Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, pamoja na mkurugenzi wa wilaya hiyo, Sheila Lukuba kutokana na kuwafanyia fujo machinga waliokataa kufanya biashara kwenye eneo lililopangwa na manispaa.

Akizungumza leo Jumanne Juni 15, 2021 katika mkutano wake na vijana uliofanyika mkoani Mwanza, Rais Samia amemwagiza Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu kutekeleza agizo lake la kutengua uteuzi wa viongozi hao.

"Kutokana na kutengewa eneo lililo nje lisilofikiwa na wateja, wamachinga Morogoro waliamua kurejea mjini na mamlaka ikaingilia kati kuwaondoa. Sijafurahia jinsi walivyotendewa na DC na mkurugenzi hawana kazi."

"Kwa sababu kuna njia nzuri zaidi ambayo ingetumika kushughulikia hilo..., sio ile iliyotumika. Sijafurahishwa nakuagiza Waziri wa Tamisemi shughulikia hilo," amesema.

Habari Kubwa