DPP Biswalo asita kuzungumzia maombi ya Rugemalira

03Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Tabora
Nipashe
DPP Biswalo asita kuzungumzia maombi ya Rugemalira

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga amesema hawezi kizungumzia suala la mshtakiwa James Rugemalira kuhusu maombi aliyoyatoa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusiana na mashitaka yanayomkabili.

Akizungumza mjini Tabora leo Jumanne, Machi 3, 2020 amesema suala hilo litapata majibu yake mahakamani ambako Rugemalira ametoa maombi yake.

"Siwezi kueleza kama alikuwa sahihi au sio kwa aliyoeleza mahakamani na suala la.mahakamani litajibiwa mahakamani," amesema Biswalo.

DPP Biswalo alikuwa na ziara ya kutembelea mahabusu na magereza na kuzindua kamati ya Jukwaa la Jinai Mkoa wa Tabora.

Habari Kubwa