JPM atoa siku saba wazabuni kulipwa

19Jan 2021
Restuta Damian
Bukoba
Nipashe
JPM atoa siku saba wazabuni kulipwa

RAIS John Magufuli ametoa siku saba kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),   kuzilipa kampuni binafsi zilizosambaza vifaa vya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana ya Ihungo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi mwaka 2016.

Rais Dk. John Magufuli akikagua madarasa ya Shule ya Sekondari Ihungo jana ambayo ilijengwa upya mara baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016 mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

Shule ya Sekondari ya Ihungo imefanyiwa ukarabati kwa kujenga majengo mapya na machache kwa gharama ya Sh. bilioni 10.9 zikiwamo Sh. bilioni 6.1 zilizotolewa kwa ufadhili kutoka Serikali ya Uingereza na Sh. bilioni 4.8 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.  

Ujenzi mpya umefanywa kwa majengo matatu ya ghorofa yenye jumla ya vyumba 24 vya madarasa, mabweni 3, vyoo na nyumba 30 za walimu na kwamba  ukarabati mkubwa umefanyika kwenye maabara 3, karakana na mifumo ya maji, umeme na taka.

Akizungumza jana baada ya uwekaji jiwe la msingi katika Chuo cha Mamlaka ya Ufundi Stadi VETA), mkoani Kagera na uzinduzi wa majengo ya Shule ya Ihungo, Rais Maguli alisema bado kuna malalamiko ya kutolipwa kampuni zilizosambaza vifaa vya ujenzi huo.

Alisema watu walikuwa wakitumia nguvu kazi zao kusambaza vifaa vya ujenzi wa majengo ya shule hiyo mpaka kufikia hatua ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwake kwamba hawajalipwa.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com  

Habari Kubwa