Katambi awahidi wananchi wa Shinyanga kuwaletea maendeleo

27Oct 2020
Marco Maduhu
Shinyanga.
Nipashe
Katambi awahidi wananchi wa Shinyanga kuwaletea maendeleo

Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia tiketi ya CCM, Patrobas Katambi, ameendelea na kampeni zake za kunadi sera kwa wananchi wa jimbo hilo, na kuahidi kuwaletea maendeleo endapo wakimchagua kuwa mbunge.

Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga mjini (CCM)Patrobas Katambi akinadi sera kwa wananchi wa Kambarage na kuomba wamchague Oktoba 28 kwa mbunge wao ili awaletee maendeleo.

Akiwa kwenye Kata ya Kambarage jana Katambi, alisema akishachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha mji wa Shinyanga unabadilika kimaendeleo na kukua kiuchumi, pamoja na kuboresha sekta ya afya, elimu, miundombinu ya barabara, ujenzi wa masoko ya kisasa, stendi ya mabasi, maegesho ya malori na ujenzi wa chuo kikuu.

“Naombeni wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini, siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, mnipigie kura nyingi za ushidi ili niwe mbunge wenu pamoja na madiwani wote wa CCM na mgombea urais John Magufuli, ili tukafanye kazi kama timu moja na kuwaletea maendeleo,” alisema Katambi na kuongeza;

“Mimi nitakuwa mbunge wa kazi tu na siyo porojo, hivyo ni chagueni ili muone kama sitawaletea maendeleo, mnipime kwa miaka mitano muone kazi yangu, nilikuwa Mkuu wa Wilaya Dodoma makao makuu ya nchi nadhani mmejionea kazi niliyoifanya ya maendeleo, hivyo hivyo nitakavyo ubadilisha mji wa Shinyanga,” alisema 

Pia Katambi aliahii kushughulika na watumishi wa afya ambao siyo waaminifu, wanaowaambia wagonjwa wenye kadi za bima ya afya CHF kuwa hakuna madawa, bali wakanunue kwenye maduka ya madawa kwa kutumia fedha zao, bila ya maelezo yoyote ya kwenda kupewa dawa bure kwenye maduka yanayotoa huduma hiyo ya CHF.

Habari Kubwa