Kortini kwa kughushi hati ya mkopo wa Milioni 350.

12Apr 2021
Hellen Mwango
Dar es Salaam
Nipashe
Kortini kwa kughushi hati ya mkopo wa Milioni 350.

MFANYABIASHARA John Kyenkungu (65) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa mashtaka mawili ikiwamo kughushi hati ya mkopo wa Sh. Milioni 350.

 Mshtakiwa ambaye pia ni Mkazi wa Magomeni, jijini alisomewa mashtaka yake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.

Wakili wa Serikali Adolf Lema alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa mashtaka mawili yote ya kughushi.

Alidai kuwa katika shtaka la kwanza tarehe na siku isiyofahamika 2014, jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya alighushi hati ya mkopo ya mwaka huo kwa kutia saini kwamba Said Nassoro amekubali kutumia hati ya nyumba yake namba 25480 ya kiwanja namba 516 kitalu B kilichopo Mikocheni Wilaya ya Kinondoni Kama dhamana ya kupata mkopo benki ya Equity ya Sh. milioni 350.

Habari Kubwa