Longido kusajili na kutoa vyeti kwa watoto 27,767

07May 2021
Zanura Mollel
Longido
Nipashe
Longido kusajili na kutoa vyeti kwa watoto 27,767

WILAYA ya Longido Mkoani Arusha, inatarajia kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano 27,767.

Hayo yameelezwa na mratibu wa zoezi la usajili na utoaji vyeti kwa watoto (RITA), ambaye pia ni ofisa ustawi wa jamii wilaya hiyo, Atunagile Chisunga, na amewataka wawezeshaji ngazi ya kutolea huduma katika vituo vya afya na kata kutowasajili na kutoa vyeti kwa watoto ambao siyo wazaliwa wa Tanzania.

"Zoezi hili litafanyika kwa siku 12, pamoja na kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano maeneo mbalimbali ya wilaya, halmashauri imejipanga kutumia kanzidata kuingiza taarifa za watoto," amesema Chisunga.

Habari Kubwa