Madiwani watatu Chadema Arusha watimkia CCM

24Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe
Madiwani watatu Chadema Arusha watimkia CCM

Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

aliyekuwa diwani wa themi katika jiji la arusha Welance Kinabo, picha mtandao

Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Madiwani hao ni pamoja na Welance Kinabo (Themi), Zakaria Mollel (Oloirien), na James Lyatuu (Unga Limited). Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dk. Maulid Madeni amethibitisha kupokea barua za madiwani hao kujiuzulu.

“Nimepokea barua zao nitatoa taarifa baaadaye,” amesema Madeni.

Hivi karibuni aliyekuwa Meya wa jiji hilo, Kalist Lazaro alijiuzulu na kujiunga na CCM. Katika uchaguzi mkuu wa 2015, Chadema kilikuwa na madiwani 25 na CCM mmoja, lakini kutokana na baadhi ya madiwani kuhamia chama hicho tawala kimekuwa na madiwani nane hadi sasa na Chadema kubakia 15.

Habari Kubwa