Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter na amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.
“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.
Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu.