Mbunge mteule anusurika kifo nyumba ikichomwa

31Oct 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Mbunge mteule anusurika kifo nyumba ikichomwa

MBUNGE Mteule wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM), amenusurika kifo baada ya nyumba ya familia yake kuchomwa moto na vijana wanaodaiwa wafuasi wa chama cha upinzani.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, alitoa taarifa hiyo jana akifafanua kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia jana nyumbani kwao na Katambi, eneo la Ushirika katika Manispaa ya Shinyanga.

Alisema moto huo ulianza kuwaka juu ya paa la choo cha nje nyumbani kwao na Katambi, mbunge mteule huyo akiwa amelala na ndugu zake.

Kamanda Magiligimba alisema walisikia kishindo kikubwa na walipoamka wakakuta moto unawaka huku pembeni kukiwa na dumu la mafuta ya petroli na baadaye wakaona vijana wawili walionekana wakikimbia na kuingia ndani ya gari.

"Baada ya kufanikiwa kuuzima moto huo, wakaona tena vijana hao wanaingia ndipo wakaanza kulifuatilia gari kwa nyuma, liliingia ndani ya Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga na kisha dereva wa gari hilo kukimbia kwa kuruka ukuta na kufanikiwa kukamatwa vijana wawili ambao walikutwa ndani ya gari," alisema.....kwa habari zaidi tembelea epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa