Membe ateuliwa Mshauri Mkuu ACT-Wazalendo

03Aug 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Membe ateuliwa Mshauri Mkuu ACT-Wazalendo

KIONGOZI  wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemteua aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa chama hicho ikiwa ni wiki tatu tangu ajiunge rasmi na chama hicho Julai 16 mwaka huu.

Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo ,Bernard Membe:PICHA NA MTANDAO

Katika taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Uenezi ,Habari na Mawasiliano kwa Umma ya chama hicho,Janeth Rithe imesema kuwa Kiongozi huyo ametumia mamlaka aliyopewa na Katiba ya chama hicho kifungu cha 83(1)(d) ambacho kinampa mamlaka ya kuteua wasahauri wa chama huku pia akimteua Emmanuel Mvula kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

“Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amemteua Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa chama” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu kitakuwa na Mkutano Mkuu kesho unaotarajiwa kujadili na kutangaza ilani ya chama hicho sambamba na kutangaza wagombea wa urais kwa pande zote mbili za muungano ingawa yapo mazungumzo yanayodaiwa kuendelea baina ya chama hicho na Chama cha ACT-Wazalendo na Chadema ili kushirikiana katika uchaguzi.

Akizungumza katika kikao cha baraza kuu leo ,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kilichofanyika Mlimani City ,Jijini Dar es Salaam  amesema kuwa chama hicho kipo katika mazungumzo na ACT-Wazalendo ili kuachiana maeneo ya kugombea ikiwemo nafasi ya Urais kwa upande wa Zanzibar.

Habari Kubwa