Mnaichafua Tanzania kupata nini jamani?

06Dec 2020
Nkwazi Mhango
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mnaichafua Tanzania kupata nini jamani?

KUMEKUWA na kampeni za makusudi za kupotosha ukweli baada ya kuisha uchaguzi mkuu wa 2020 za kuichafua, kuihujumu na kuisingizia Tanzania.

Nasema hivi kutokana na wahusika kutotoa ushahidi wowote unaoingia akilini kutokana na tuhuma zinazoendeshwa na baadhi ya Watanzania.

Mfano hivi karibuni, nilihudhuria mjadala kupitia zoom juu ya mashambulizi ya kigaidi huko Mtwara yaliyofanywa na magaidi toka Msumbiji.

Tofauti na mijadala niliyowahi kuhudhuria, huu ulionyesha wazi namna ya waliouandaa walivyolenga kulaumu serikali kwa “kutoshughulikia” kadhia hii jambo ambalo, hadi sasa, sijui kama lina chembe ya ukweli ikizingatiwa kuwa Tanzania haijawahi kuacha kuwalinda wananchi wake.

Isitoshe, madai yaliyotolewa ni makubwa mno kuwa magaidi walichoma vijiji na kuua watu ukiachia mbali kuingiza silaha za kivita nchini...........kwa habari zaidi fuatilia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa