Mwinyi ammwagia sifa Samia

12Apr 2021
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Mwinyi ammwagia sifa Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye amempongeza kwa kuanza vizuri majukumu yake ya kuongoza nchi.

Akizungumza baada ya mazungumzo yao, Rais mstaafu Mwinyi amesema amefika nyumbani kwa Rais Samia kumjulia hali, kumtia moyo na kumhakikishia kuwa yeye na Wazee wenzake wapo tayari kutoa ushirikiano na kumsaidia wakati wowote watakapohitajika kufanya hivyo.

"Mama ameanza vizuri, ingekuwa ni nyimbo ningesema once more!!!, ameanza vizuri kabisa na kila mmoja ana furaha, kila raia unayemsikia anasema Mama ameanza vizuri, tuliyekuwa nae tulikuwa na Rais mzuri sana ,mzoefu wa mambo ya kiserikali ,ametufanyia kazi nzuri sana, sasa kaacha mambo haya ghafla kamuachia mwenzie"-alisema Rais mstaafu Mwinyi.

 

Habari Kubwa