Mzee amzawadia Magufuli jogoo aahidi kumpa mama yake

30Jul 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Mzee amzawadia Magufuli jogoo aahidi kumpa mama yake

MKAZI wa kijiji cha Somanga amempa Rais John Magufuli zawadi ya kuku baada ya kueleza kufurahishwa na kazi anazofanya Rais ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji hicho pamoja na barabara katika mkoa huo.

Rais John Magufuli akiwa ameshikilia kuku aliyepewa zawadi na mkazi wa kijiji cha Somanga:PICHA NA MTANDAO

Rais Magufuli amepewa zawadi hiyo baada ya kutembelea kijiji hicho siku moja baada ya mazishi ya hayati Benjamini Mkapa aliyekuwa Rais katika Serikali ya awamu ya tatu yaliyofanyika  katika kijiji cha Lupaso wilayani Masasi Mkoani Mtwara .

“Nina kuku pale nyumbani kwangu jogoo anapata hivi ,naomba kwa mamlaka yako nikakukamatie jogoo umpelekee mama mzazi aliyekulea Dk.Magufuli aliyekufundisha vizuri ,aliyekufundisha wema na huruma kwa wanadamu “ amesema Mkazi huyo.

Akizungumza baada ya kumpokea kuku huyo Rais Magufuli alimshukuru Mzee huyo na kumpa shilingi lakini moja ,wakati huo huo Rais Magufuli amewataka wakazi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kupinga maendeleo kwa kuweka vikwazo katika maeneo ambayo Serikali inataka kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

 

Habari Kubwa