Polepole awatoa hofu walioshindwa kura za maoni

23Jul 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Polepole awatoa hofu walioshindwa kura za maoni

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakitafuti mshindi kupitia kura za maoni na kwamba kura hizo zitakisaidia tu chama hicho kuhitimisha maamuzi yake kuhusiana na watakaofaa kugombea .

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Humphrey Polepole:PICHA NA MTANDAO

Akizungumza na chombo kimojawapo cha habari nchini Polepole amesema kuwa hata wale waliofungana kwa kura katika baadhi ya majimbo kwenye kura za maoni za chama hicho uchaguzi hautarudiwa bali watapaswa kusubiri maamuzi ya vikao vya juu.

“Yapo maeneo mengine ambapo wagombea wamefungana idadi ya kura mfano kule Mwibara nafikiri ,kuna kule Sengerema sasa hii wala isiwaletee hofu kwa sababu moja hatutafuti mshindi kwenye kura za maoni kwa hio hata kama kura zimefungana hatutarudia zoezi tutaendelea na vikao vya kufanya mapendekezo” amesema Polepole

Zoezi  la kura za maoni katika chama hicho limekamilika huku baadhi ya watu mashuhuri wakianguka katika mchakato huo na sura mpya kuchomoza.

Habari Kubwa