Rais Dk. Mwinyi ameagana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo April 7, 2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC, kumuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Idrisa Mustafa Kitwana, akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, unaofanyeka Jijini Maputo Msumbuji.(Picha na Ikulu)