Rais Samia awasili nchini Kenya

04May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Rais Samia awasili nchini Kenya

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewasili nchini Kenya na kupokewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Ziara hiyo ya Rais Samia ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na itakuwa ndio ziara ya pili  tangu alipochukua madaraka kutoka kwa Hayati Dk. John Magufuli.

Rais Samia anatarajia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi.

Alifanya safari yake ya kwanza akiwa Rais nchini Uganda mnamo Aprili 11 na Rais Yoweri Museveni akielezea kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda

Habari Kubwa