Serikali yaombwa kuingilia kati suala la uuzaji mafuta

13Jul 2020
Katavi
Nipashe
Serikali yaombwa kuingilia kati suala la uuzaji mafuta

WAENDESHA vyombo vya moto katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Wameiomba serikali kuingilia kati swala la uuzaji wa mafuta ya Petroli kutokana na vituo vingi vya uuzaji wa mafuta hayo kugoma kutoa huduma hiyo.

Foleni ya madereva wakisubiri mafuta katika kituo cha kuuzia mafuta katika kituo cha kuuzia mafuta katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, leo madereva hao walisema wanapoteza muda mwingi kupanga foleni kusubiri mafuta yanayotolewa na kituo kimoja katika Manispaa hiyo.

Doto Julius ni Dereva wa gari ya kutoka Mpanda kwenda Kasekese ambaye alisema wakienda kununua mafuta kwenye baadhi ya vituo wanaambiwa hawauzi mafuta hayo hali yakuwa mafuta yapo.

"Tunapata shida sana tunaenda kununua mafuta tunaambiwa hawauzi sijui ni kwasababu ya bei hadi ipande hatujui wengine wana mafuta kabisa lakini hawataki kuuza" amesema Julius.

Meneja wa kituo Cha mafuta Sereniva Thomas Magabe amesema kituo hicho kwa sasa kimekuwa Kama mkombozi kwa madereva kutokana na vituo vingi kukosa mafuta kwa kipindi hiki.

Kwa upande wake Afisa huduma kwa wateja na Utawala mkoa wa Rukwa Ramadhan Kakende amesema kuwa suala hilo kwa mkoa wa Katavi ndio anaisikia kwa mara ya kwanza,hivyo mpaka afanye mawasiliano na viongozi wa juu.

Hata hivyo alisema tatizo kama hilo liliwahi kutokea katika mkoa wa Rukwa na baada ya kufanya utafiti walitambua kuwa wamiliki wa vituo hivyo wanakwamishwa na vituo vikubwa vya mafuta vilivyopo jijini Dar es Salaam ambapo wakituma magari yao wanakataa kuwawekea mafuta.

Habari Kubwa