Taharuki yatanda madai wanafunzi kuchanjwa chanjo ya corona

30Jul 2021
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Taharuki yatanda madai wanafunzi kuchanjwa chanjo ya corona

TAHARUKI imeibuka katika Shule mbili za Msingi zilizopo Mtaa wa Tegeta Jijini Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kuwepo kwa chanjo kwa wanafunzi wa shule hizo kinyume na msimamo wa Serikali wa chanjo kwa hiari kwa kila anayehitaji.

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KUNDUCHI.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kunduchi na Shule ya Msingi Pius Msekwa jana walikimbia masomo na kurudi nyumbani wakidai kuwepo kwa chanjo ya lazima kwa kila mwanafunzi jambo ambalo liliibua taharuki baada ya wazazi wa wanafunzi hao kufika katika shule hizo kutaka kupata ukweli wa jambo hilo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Mohamed Mawala akiongea na mwandishi wetu jana, alisema kuwa suala hilo halina ukweli na kuwataka wazazi kuondoa hofu kwa kuwa chanjo ni hiyari kama ilivyoelekezwa na Serikali na hakuna atakayelazimishwa.

 

Habari Kubwa