Akiongea na chombo kimojawapo cha habari nchini, Nasir Abubakari amedai kuwa Membe ni mtu makini na mwenye busara anayeweza kuongoza mabadiliko makubwa ya kiuongozi nchini.
“Kitendo walichomfanyia Chama cha Mapinduzi kumfukuza uanachama ni kumdhalilisha ,mtu ambaye amekuwa mtumishi wa Serikali kwa kipindi kisichopungua miaka 40” amedai Abubakari.
Kauli ya wanachama hawa inakuja wakati ambapo tayari Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe amekwisha mkaribisha Membe kujiunga na upinzani nchini ili kuleta nguvu ya kusaidia kuleta mabadiliko.