“Sitaki kuona mtoto wa Kitanzania anasomea chini ya mti wala anakaa chini, nataka watoto wote wasomee madarasani na wakae kwenye madawati nataka kuona mazingira ya kujifunzia yanaboreshwa." - Ummy
Ameongeza kuwa hafurahii namna ambavyo wanafunzi wanasoma kwa zamu, wengine wanaenda shule asubuhi na wengine mchana kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.