“Tusaidieni kuwapata watoto wetu’

16Jul 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
“Tusaidieni kuwapata watoto wetu’

RAMADHANI Mlinda, mwenye miaka miwili ametoroshwa na mtu ayejifanya shangazi yake aitwaye Fatuma, aliyemchukua nyumbani kwa mama yake Tandale kwa Tumbo jijini Dar es Salaam.

Shangazi wa mtoto Hadija Mlinda, aliiambia Nipashe kuwa udanganyifu huo wa kumpora mtoto ulitokea Jumatano wiki hii nyumbani kwao, akiwa na ndugu zake, baada ya mgeni huyu kuwahadaa kuwa ni shangazi wa Ramadhani.

Alisema baada ya kuruhusiwa kumsalimia mtoto aliondoka naye hadi sasa ametafutwa na ndugu zake bila mafanikio.

Baada ya kuwasiliana na baba mzazi Bakari anayeishi Kigogo alisema hamfahamu aliyemwiba mwanaye na hata Fatuma ambaye ni dada wa Bakari ni mgonjwa ameumia mguu na hadi sasa hajaweza kutembea.

Hivyo hadi sasa haijafahamika aliyemchukua mtoto huyo.

Baada ya kutoa taarifa kituo cha Magomeni walifungua jalada namba MAG/RB/75296/2017na juhudi za kumtafuta zinaendelea wanaomba kwa yeyote atakayemwona atoe taarifa kituo chochote cha polisi au awasiliane kwa namba 0716- 841688 au 0657- 136612.

Wakati huohuo, mtoto Lukumani Yusufu (15) anayeishi Kinondini Mkwajuni Dar es Salaam, anatafutwa na ndugu zake, baada ya kutoweka nyumbani kwao akihofia kupigwa na baba yake.

Alikimbia alipoanza kuulizwa maswali ya shule, juhudi za kumtafuta zinafanyika na ndugu zake wanaomba yeyote atakayemwona atoe taarifa kituo chochote cha polisi au apige simu kwenda 0657- 449775 au 0659- 344671. Taarifa za kutweka kwako zimefikishwa polisi kwenye jalada KH/RB/109/2017.