"2020 upinzani kuchukua nchi mapema"-Lowassa

14Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
"2020 upinzani kuchukua nchi mapema"-Lowassa

WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amehudhuria kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Muriet mkoani Arusha huku akitaka upinzani kuchukua nchi mwaka 2020.

“Nimekuja kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Muriet, Simon Moses Mollel, (Chadema) mpeni kura nyingi za ushindi,” alisema.

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Muriet, uliofanyika eneo la sokoni kwa Mrombo jijini Arusha.

“Nawashukuruni mwaka 2015, mlinipa kura nyingi zaidi ya milioni sita, Watanzania mlinipa kura nyingi sana mpaka mkanitungia jina la Rais wa mioyo ya watu,”..........Nasema watusubirie mwaka 2020 tutawaonyesha kazi, lazima tuchukue nchi mapema.”