2025 wanawake tutamuweka rais mwanamke - Rais Samia

15Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
2025 wanawake tutamuweka rais mwanamke - Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 wanawake watamuweka madarakani rais mwanamke.

"Wanawake bado hatujaweka rais mwanamke, rais huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na matakwa ya katiba, tulichochangia sisi na dada zetu na mama zetu ni ile kusukuma hadi mwanamke akawa makamu wa Rais ule ndio mchango mkubwa tulioufanya wanawake, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, " amesema.

Rais Samia amesema hayo leo Septemba 15, 2021 alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya demokrasia dunia.

“Sasa ndugu zangu rais mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameaanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia," amesema.

Habari Kubwa