56 washikiliwa na Jeshi la Polisi tuhuma wizi wa magari, pikipiki

20Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
56 washikiliwa na Jeshi la Polisi tuhuma wizi wa magari, pikipiki

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wapatao 56 wanaotuhumiwa kujihusisha na makosa ya wizi wa magari na pikipiki.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Hayo yameelezwa Leo na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema, Katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, 2021 Jeshi la polisi limefanya operesheni mbalimbali ya kupambana na waharifu vinara wanaojihusisha na wizi wa magari pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es salaam.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema kuwa bado Jeshi linaendelea na uchunguzi na watuhumiwa wanaendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi.

Habari Kubwa