Asifia mavazi wabunge wanawake, aomba dawati la wanaume

10Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
Asifia mavazi wabunge wanawake, aomba dawati la wanaume

MBUNGE wa Nyang’wale (CCM), Hussein Amar ameomba mwongozo wa Spika kuhusu mambo mawili ambayo ni; kuwapongeza wabunge wanawake kwa mavazi mazuri wanayoyavaa bungeni kwa sasa pamoja na kuomba Serikali ianzishe dawati la wanaume.

MBUNGE wa Nyang’wale (CCM), Hussein Amar.

Mbunge huyo ameomba muongozo huo leo Alhamisi, Juni 10, 2021 aliposimama kusifia mavazi mazuri yenye staha ambayo wabunge wanawake wameanza kuvaa akisisitiza huo ni mfano wa kuigwa.

“Spika ukinipa nafasi niwape zawadi baadhi ya wabunge wanawake hapa maana kweli wamevalia vizuri na huu ni mfano wa kuigwa maeneo yote,” amesema Amar.

Itaumbukwa kuwa siku za hivi karibuni Mbunge wa Momba (CCM),  Condesta Sichalwe alitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Spika Job Ndugai kutokana na kuvaa vazi lililodaiwa lisilokuwa na staha.

Kuhusu dawati la wanaume ameomba wabunge wanawake wasaidie katika majimbo yao ili kuanzishwe dawati la wanaume kwa kuwa kuna uonevu wanaokumbana nao.

Habari Kubwa